Mufti
mkuu wa Tanzania Sheikh Alhaji Abubakari Zuberi ameivunja mamlaka ya
uendeshaji na usimamizi wa msikiti mkuu wa mkoa wa Arusha na kuweka
mamlaka mpya ili kuimarisha utendaji.
Akitangaza
maamuzi hayo kwa niaba ya mufti Sheikh mkuu wa mkoa wa Arusha Shabani
Juma alisema anaamini kuwa mamlaka mpya iliyowekwa itafanya kazi kwa
ufanisi na kwa kasi ya hali ya juu pamoja na kujipanua ili kwafikia
waumini wengi kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwahudumia kwa
ukaribu.
Hata
hivyo baadhi ya wajumbe wa mamlaka iliyovunjwa wamesema kuwa
hawajaridhishwa na uamuzi huo kwani hawakushirikishwa wakati wa vikao
vya maamuzi vya mkoa vilivyojadili majina kumi na tano ya wajumbe
yaliyotumwa kwa mufti kwa ajili ya uteuzi huo wa mamlaka mpya.
Kwa
upande wao wajumbe wapya waliochaguliwa kuingia katika mamlaka hiyo
mpya wamesema kuwa wanachangamoto kubwa ya kuwaunganisha waumini pamoja
na viongozi wao ili kuleta maendeleo na kudumisha mshikamano.
No comments:
Post a Comment