NICK JONAS ACHOMOA KUTOKA NA KENDALL - LEKULE

Breaking

25 Aug 2015

NICK JONAS ACHOMOA KUTOKA NA KENDALL


Nick Jonas na Kendall Jenner.
New York, Marekani
NICK Jonas na Kendall Jenner awali baada wa kuripotiwa kuwa wanatoka kimapenzi, iliaminika kuwa ingekuwa bonge la kapo, lakini ghafla msanii wa muziki na muigizaji huyo, kachomoa kuwa wala hatoki na mwanadada huyo.

Nick Jonas .
Kendall ambaye ni mdogo wa mtangazaji wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian, amewahi pia kuripotiwa kutoka na mkali wa Langalanga, Lewis Hamilton.
Nick ambaye ana vipaji vingi vikiwemo kuigiza, kuimba na mwandishi wa nyimbo, mapema wikiendi iliyopita, aliibuka na kusema kuwa Kendall ni msichana mrembo sana lakini hawatoki kimapenzi japokuwa wamekuwa wakionekana pamoja.
Nick aliyazungumza hayo wakati akiwa kwenye mahojiano na kipini cha TV mwishoni mwa wiki iliyopita na kusema kuwa akili yake kwa sasa ipo kwenye kazi zake za muziki."Ni msichana mzuri lakini hatupo kimapenzi," alisema Nick wakati akiipromoti singo yake ya ‘Levels.’

No comments: