Waziri
Mkuu mstaafu ambaye juzi alichukua kadi ya uanachama wa Chadema,
Frederick Sumaye ameukosoa uamuzi wa rais John Magufuli kuwasamehe watu
waliorejesha kiasi cha fedha walichokwepa kulipa kodi.
Sumaye
alitoa mtazamo wake huo juzi jijini Arusha baada ya kukabidhiwa kadi
ya uachama wa Chadema ikiwa ni miezi takribani mitatu tangu alipojiunga
na harakazi za Ukawa na kutangaza kuihama CCM.
“Unawezaje
kutoa msamaha kwa wezi na wakepa kodi nchini kwa kuwapa siku saba eti
wawe wamelipa madeni yao? Hili ni jambo la ajabu kabisa. Unawezaje
kupitisha msamaha kwa wezi na wakwepa kodi? Sumaye alihoji.
“Haya tuliyaona wakati wa sakata la EPA na sasa tunayaona kwenye makontena, wezi wanasamehewa,” aliongeza.
Zaidi
ya shilingi bilioni 10 zimekusanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)
kutoka kwa wafanyabishara mbalimbali waliokwepa kodi kupitia makontena
yaliyotoroshwa bandarini baada ya rais kutoa siku saba za ‘rehema’.
Baada
ya siku hizo kupita (ijumaa), hivi sasa serikali inawasaka
wafanyabiashara 15 ambao hawakujisalimisha katika kipindi kilichotolewa
na rais Magufuli. TRA imeahidi kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yao
kama rais alivyoagiza.
No comments:
Post a Comment