Picha ya
"Dokuz 8 Haber" inayoonyesha jinsi mlipuko ulivyotokea katika umati wa
watu waliokua wakiandamana kwa amani, Oktoba 10, 2015 katika mji wa
Ankara, Uturuki.
Serikali
ya Uturuki imelitaja Jumatatu wiki hii, kundi la Islamic State (IS) kama
mtuhumiwa namba 1 wa mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyotokea wiki
iliyopita katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara.
Mashambulizi
hayo yaliwaua watu wasiopungua 97 na kusababisha mgawanyiko nchini
Uturuki huku baadhi ya raia wakipinga serikali ya Rais Recep Tayyip
Erdogan.
Siku
mbili baada ya mashambulizi mabayayaliyosababisha vifo vya watu wengi
nchini Uturuki, Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu pia alithibitisha kuwa,
licha ya majonzi na mvutano viliyoibuka, uchaguzi wa haraka wa bunge
utafanyika tarehe 1 Novemba vizuri.
" Kama
unaangalia jinsi shambulio hilo lilivyotekelezwa, tunatakiwa kuichukulia
Daech (neno fupi la Kiarabu linalomaanisha kundi la IS) kama adui wetu
namba 1chetu ", Davutoglu amesemakwenye runinga ya NTV.
" Tuna jina la mtu ambaye anatuelekeza kwenye na kundi hilo ", ameongeza Davutoglu.
Jumamosi
asubuhi Oktoba 10, watu wawili walijilipua mbele ya kituo kikuu cha
treni katika mji mkuu wa Uturuki katikati ya umati wa watu waliokua
wameitikia wito wa vyama vya wafanyakazi, mashirika yasio ya kiserikali
na vyama vya mrengo wa kushoto na kusababisha watu 97 kuuawa.
Wanaharakati hao walikua wakiandamana wakipinga kuanzishwa kwa mapigano
kati ya jeshi la Uturuki na waasi wa Kishia wa Huthi.
Ripoti ya
mwisho, ambayo bado ni ya muda, iliyochapishwa na viongozi wa Uturuki
inaonyesha kuwa watu 97 walifariki na wengine 507 walijeruhiwa, ikiwa ni
pamoja na majeruhi 65 ambao wako katika hali mbaya.
Hata kama
amelinyooshea kidole kundi la Islamic State, Ahmet Davutoglu , hata
hivyo, amewataja waasi wa Kikurdi wa (PKK) au waasi wa DHKP-C, ambao
amesema kuwa ni washukiwa wa kubwa wanaoendesha mashambulizi mbalimbali
nchini Uturuki.
Kwa
mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, wachunguzi wanaamini kwamba
kifaa kiliyolipuka katika mji wa Ankara ni aina moja na kile
kiliyotumiwa katika shambulio la Suruç (Kusini) mwezi Julai.
No comments:
Post a Comment