Kikosi cha Kenya cha Olimpiki chatajwa - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Sunday, 3 July 2016

Kikosi cha Kenya cha Olimpiki chatajwa


Kamati ya olimpiki nchini Kenya, Nock, na shirikisho la riadha nchini Kenya, AK, zimetaja timu itakayoiwakilisha Kenya mjini Rio, nchini Brazil Agosti mwaka huu.

Ingawa wanariadha wawili wa kwanza katika kila kitengo walijanyakulia tiketi, Kikosi cha Kenya pia kimeangazia masuala mengine kama vile fomu ya wanariadha, matokeo yao katika mbio za riadha duniani yakiwemo mashindano ya hivi karibuni ya riadha nchini Afrika Kusini.

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Olimpiki katika mbio za mita mia nane, David Rudisha, amepewa fursa nyingine ya kushiriki katika Olimpiki licha ya kubwagwa na Alfred Kipketer.

Licha ya kujiondoa kutoka mbio za mita elfu kumi, bingwa wa Dunia, Geodfrey Kamworor ni miongoni mwa wanariadha watakaowania medali katika mbio hizo ifikapo Agosti. Kamworor, na Bedan Karoki wataungana na mshindi wa mbio za majaribio Paul Tanui, na mwenzake Charles Yosei aliyenyakua nafasi ya pili.

"Ninafuraha kubwa kuiwakilisha Kenya Katika Olimpiki. Natarajia nitafanya vyema katika mashindano ya Olimpiki," alisema Tanui.

Katika mbio za mita mia nane, upande wa kina dada, mshindi wa mbio za majaribio Margaret Nyairera Wambui, anatarajia ushindani mkali kutoka Eunice Sum, na Winnie Chebet wakati watakapokutana kwenye olimpiki licha ya kuwabwaga katika mbio za majaribio.

Hata hivyo Kenya inatarajia ushindani mkali kutoka kwa Caster Semenya.

"Ni majivuno makubwa kufuzu na naamini hakuna mtu asiyeweza kushindwa, nia yangu ni kuondoka na dhahabu, alisema mshindi wa mbio za majaribio, Margaret Nyairera.''

Kwa upande wa mbio za mita mia nne kuruka vihunzi, bingwa wa dunia Nicholas Bett na pacha wake, Aaron Koech waliitwa kwenye timu hiyo. Kujumuishwa kwa Bett kuliwashangaza wengi kwani hakushiriki kwenye majaribio.

Bingwa wa mbio za mita elfu tano na elfu kumi upande wa wanawake, Vivian Cheruiyot, alitajwa katika timu zote mbili ambapo analenga kuwania katika vitengo vyote viwili.
Wengine waliotajwa ni mrusha mkuki, Julius Yego, ambaye atakuwa mwakilishi pekee wa Kenya katika mashindano ya Rio.

''Tunawapongeza wote waliofuzu, na wakati huu tunatarajia kujiandaa ipasavyo ili kufanya vyema katika mashindano ya Rio," alisema rais wa riadha nchini Kenya, Jackson Tuwei.

ORODHA KAMILI - WANAUME 200m: Kevin Nkanata, Mike Mokamba 400m Hurdles: Nicholas Bett, Boniface Mucheru, Aron Koech 400m: Alphas Kishoyan, Raymond Kibet, Alex Sampao, Boniface Mweresa 800m: Alfred Kipketer, Ferguson Rotich, David Rudisha 1500m: Asbel Kiprop, Elijah Manangoi, Ronald Kwemoi 3000m S/Chase: Brimin Kipruto, Conceslus Kipruto, Ezekiel Kemboi 5000m: Caleb Mwangangi Ndiku, Isaiah Kiplangat Koech 10000m: Paul Tanui, Charles Yosei, Geoffrey Kamworor, Bedan Karoki Marathon: Eliud Kipchoge, Stanley Biwott, Wesley Korir Kurusha mkuki: Julius Yego Kutembea 20km: Samuel Gathimba, Simon Wachira High Jump: Mathew Sawe


ORODHA KAMILI WANAWAKE 400m Hurdles: Maureen Jelagat 400m: Maureen Jelagat, Margaret Nyairera Wambui 800m: Margaret Nyairera Wambui, Eunice Sum, Winnie Chebet, 1500m: Faith Chepngetich, Nancy Chepkwemoi. Viola Lagat 3000m S/Chase: Hyvin Kiyeng, Beatrice Chepkoech, Lydia Rotich 5000m: Vivian Cheruiyot, Hellen Obiri, Mercy Cherono 10000m: Vivian Cheruiyot, Betsy saina, Alice Aprot Marathon:Jemima Sumgong, Helah Kiprop, Visline Jepkesho Kutembea 20km: Grace Wanjiru
Post a Comment