Wapiganaji
wa kikurdi, wanaoungwa mkono na waasi wa kiarabu, wamefanyikiwa
kuwaondoa wanamgambo wa IS katika maeneo mengi ya Syria.
Jeshi la
Marekani limetoa zaidi ya tani 45 za silaha kwa waasi wanaopambana na
wanamgambo wa Islamic State (IS) kaskazini mashariki mwa Syria.
Jeshi hilo liliangusha shehena ya vifaa katika jimbo la Hassakeh, Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Marekani ameeleza.
Shehena hizo zimeripotiwa kuhusisha silaha ndogo ndogo,kubwa na maguruneti.
Hatua
hiyo imekuja siku kadhaa baada ya Marekani kuacha mpango wa gharama ya
dola za marekani milioni mia tano wa kuwafundisha maelfu ya waasi
kupambana na IS
Badala
yake imeelezwa kuwa fedha hizo zitatumika kugharimia silaha ambazo
zitakuwa zinahitajika kwa makamanda wa makundi ya waasi ambao wako
katika maeneo ya mapambano.BBC
No comments:
Post a Comment