Straus Kahn na mkewe akitoka mahakamani
Aliyekuwa mkuu wa shirika la fedha duniani IMF,Dominique Strauss Kahn ameshtakiwa nchini Ufaransa na mashtaka ya usaidizi wa kuwanunua wanawake ili kushiriki katika sherehe za ngono.
Bwana Straus Kahn ambaye alitabiriwa kushinda uchaguzi wa urais nchini Ufaransa alilazimika kukata harakati zake za kisiasa baada ya kudaiwa kum'baka msichana mmoja msaidizi.
Bwana Straus-Kahn amekana kujua kwamba wanawake katika sherehe hiyo walilipwa.
Mwandishi wa BBC mjini Paris amesema kuwa kesi hiyo ni jaribio la kubadilisha mitazamo ya kimaadili nchini Ufaransa.
Straus Kahn na mwanamke msaidizi ambaye alidai kunyanyaswa kijinsia na Kahn
No comments:
Post a Comment