Rais wa Nigeria anusurika bomu - LEKULE

Breaking

2 Feb 2015

Rais wa Nigeria anusurika bomu



Bomu limelipuka kazkazini mwa Nigeria nje ya uwanja mmoja wa soka ambapo rais Goodluck Johnathan alikuwa amehutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi.

Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuko huo ulitokea katika eneo moja la kuegesha magari dakika chache tu baada ya rais huyo kuondoka katika uwanja huo uliopo mji wa Gome.

Bwana Johnathan anafanya kampeni za kutaka kuchaguliwa tena katika uchaguzi unaotarajiwa tarehe 14 mwezi Februari,lakini anakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama kutoka kwa kundi la Boko Haram huku kundi hilo likiimarisha mashambulizi yake.

No comments: