WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema hana kinyongo na mtu yeyote kwa sababu
alitangaza msamaha siku aliyokabidhiwa cheti kuwa Mbunge wa Jimbo la
Ruangwa na kusisitiza kuwa siasa ziliisha tangu Oktoba 25, mwaka huu.
Alitoa
kauli hiyo juzi jioni wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika
kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
mikutano wa Likangala wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
“Sina
kinyongo na mtu yeyote na roho yangu iko huru, hivi ndiyo nilivyo.
Nilikwishatangaza msamaha kwa hiyo ninawaomba wale niliowakwaza nao pia
wanisamehe… lakini ninawasihi kuwa milango iko wazi, wawe huru kurudi
wakati wowote,” alisema huku akishangiliwa na wananchi hao.
Aliwaeleza
wakazi hao wa Ruangwa na vitongoji vyake kwamba amekuja kuwashukuru kwa
kumchagua na kumpa kura nyingi la sivyo asingefanikiwa kuwa mbunge
wao.
“Kipekee ninamshukuru Mungu aliyemuongoza Mheshimiwa Rais na kutupa sisi wana Ruangwa tusaidiane kulibeba jukumu hili.
"Ninawahakikishia
kuwa pamoja na jukumu hili la kitaifa, sitawaacha wala sitawaangusha.
Nitakwenda mikoa mingine hapa nchini ili kuwasikiliza na kuwahudumia
Watanzania huku nikijua kwamba mpo salama.”
No comments:
Post a Comment