GILBERTO Benitez Zarate wa Paraguay amekamatwa akishitakiwa kwa kumbaka na kumpa ujauzito binti yake wa kambo mwenye umri wa miaka 10.
Zarate aliyekamatwa baada ya kutoroka na kujificha kwa zaidi ya wiki mbili na kusababisha mgogoro mkubwa wa kitaifa kwa vile mama yake anataka ujauzito huo utolewe, alikamatwa Mei 9 mwaka huu.
Mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 42 anayekabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela, amekana kosa hilo na kusema anasingiziwa na rafiki yake wa kike, ambaye ni mama wa binti huyo, kwa vile alimtishia kumwacha.
“Niko tayari kufanya kipimo chochote kuonyesha si mimi niliyefanya hivyo. NImetembea na wanawake kibao lakini kamwe hakuna niliyempa mimba,” alisema Zarate katika mahojiano, ambapo tukio hilo limezua mjadala mkali katika mabunge mawili ya nchi hiyo.
Utoaji mimba kwa mila za Kanisa Katoliki ni kitendo cha jinai, labda tu pale ambapo maisha ya mwanamke husika yakiwa hatarini.
Ujauzito wa msichana huo uligundulika Aprili 21 wakati mama yake alipompeleka hospitalia kiamini alikuwa na uvimbe tumboni. Mama huyo amekamatwa akiaminika alisababisha kudhalilishwa kwa binti yake huyo.
No comments:
Post a Comment