Rais Shein ametangaza Baraza la Mawaziri, wamo watatu wa upande wa upinzani - LEKULE

Breaking

10 Apr 2016

Rais Shein ametangaza Baraza la Mawaziri, wamo watatu wa upande wa upinzani



April 9 2016 Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein ametangaza Baraza la Mawaziri lenye Mawaziri 13 na Manaibu waziri 7 ambapo watatu wametoka upande wa upinzani ambao ni Hamadi Rashid amekuwa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi  pamoja na Juma Ally Khatib na Said Sud Said wamekuwa Mawaziri katika wizara Maalum.
MAWAZIRI 
Issa Haji Ussi – Waziri Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Haruna Ali Suleiman – Waziri wa Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
Abdi Omary Kheri – Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI na Idara Maalum
Mohamed Abood Mohamed – Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Dkt Khalid Salim Mohamed – Waziri wa Fedha na Mipango
Mahamoud Thabit Kombo – Waziri wa Afya
Riziki Pembe JUma – Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Balozi Amina Salum Ali – Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko
Balozi Ali Abeid Karume – Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Rashid Ally Juma – Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
Hamad Rashid Mohamed – Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Nurdin Kastiko – Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto
Salama Abood – Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira
MANAIBU WAZIRI 
Harusi Said Suleiman – Wizara ya Afya
Mmanga mjengo Mjawili – Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Mahamed Ahmed Salum – Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Lulu Mshamu Khamis – Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Chum Kombo Khamis – Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo
Juma Makungu Juma – Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira
Khamis Juma Maalim – Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

No comments: