Mkali wa muziki wa dansi aliyefanya vizuri akiwa na bendi ya FM Academia na Stono Musica, Ndanda Kosovo ambaye
alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo ambapo alilazwa katika
hospitali ya mwananyamala na baada ya hali yake kuwa mbaya alihamishiwa
katika hospitali ya Muhimbili.
April 09 2016 zimeripotiwa habari za kifo chake na millardayo.com imepata nafasi ya kuzungumza na Baba mdogo wa mwanamuziki huyo, Kardinal Gental ambaye amethibisha kifo chake>>>’Ni
kweli kabisa ndanda amefariki nilikuwa naye jana muhimbili tangu
asubuhi mpaka usiku tumekesha naye pale mpaka leo saa moja asubuhi mke
wake alipokuja mimi nikaondoka nikaacha anamlisha lakini baadaye
wakanitumia taarifa taarifa kwamba ndanda amefariki’.
>>>>’Kitu
kikubwa kilichomuondoa Ndanda ni vidonda vya tumbo kwani alikuwa
akitapika mpaka kuna chembechembe za damu zilikuwa zinatoka‘
No comments:
Post a Comment