MIKUTANO YA BENKI YA DUNIA NA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA INAZIDI KUPAMBA MOTO -LIMA - LEKULE

Breaking

11 Oct 2015

MIKUTANO YA BENKI YA DUNIA NA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA INAZIDI KUPAMBA MOTO -LIMA



 Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi akiwa na Mchumi mwambata Bw. Paul Mwafongo Kushoto pamoja na  Afisa Mawasiliano Wizara ya Fedha Bi. Eva Valerian kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja katika eneo la mikutano ya kimataifa ya Benki ya Dunia na shirika la fedha la kimataifa nchini Peru- Lima.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali  Dr. Servacius    Likwelile wa pili kutoka kulia ( kwa nafasi ya uwaziri na Ugavana wa Benki ya Dunia) akiwa kwenye picha ya pamoja ya Mawaziri wa Fedha wa  nchi  20 wanachama ( V20 - Vulnerable Twenty) watakao asirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi (climate change).Mawaziri hao wanatoka nchini Afghanistan, Bangladesh, Barbados, Bhutan, Costa Rica, Ethiopia, Ghana, Kenya, Kiribati, Madagascar, Maldives, Nepal, Philippines, Rwanda, Saint Lucia, Tanzania, Timor-Leste, Tuvalu, Vanuatu and Vietnam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile aliyeweka kidole shavuni akiwa pamoja na ujumbe wa Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Fedha wakiwa katika ufunguzi wa mkutano wa kundi la nchi 20 zitakazo athirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.
  Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile wa pili kulia akitoa ufafanuzi kwenye majadiliano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop kushoto na Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu Bi. Mamta Murth kushoto kwake. Kutoka kulia ni  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi, na baada ya katibu Mkuu  kulia kwake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natujwa Mwamba.
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini mafunzo ya namna ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile wakiwa katika semina ya mafunzo ya namna ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha.

 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu akitoa ufafanuzi katika majadiliano hayo pamoja na ujumbe wa Tanzania nchini Peru –Lima.



Baadhi ya ujumbe wa Tanzania wakijadiliana yaliyojiri kwenye mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inayoendelea nchini Peru. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi, Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade, Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya na Mchumi Mwambata wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Paul Mwafongo.

No comments: