Wanajeshi wa Chad, Boko Haram,wapambana - LEKULE

4 Feb 2015

Wanajeshi wa Chad, Boko Haram,wapambana



Kumekuwa na mapigano makali kati ya Vikosi vya Chad na Wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.Msemaji wa Jeshi la Chad amesema vikosi vyake ambavyo ni sehemu jeshi la kimataifa wamepambana na Boko Haram mjini Gamboru, katika eneo la mpaka wa Nigeria na Cameroon.

Taarifa zinasema Wanajeshi tisa wa Chad na takriban wanamgambo wa Boko Haram 200 wameuawa, lakini idadi ya wanamgambo wanaodaiwa kuuawa haijathibitishwa.

Boko haram wamekuwa wakipambana na Vikosi vya Cameroon upande wa pili wa Mpaka, mjini Fotokol nchini humo.

No comments: