Utalia mpaka lini kisa mapenzi? - LEKULE

Breaking

3 Feb 2015

Utalia mpaka lini kisa mapenzi?



... Zingatia thamani kubwa ya chozi lako!
Acha Mungu aitwe Mungu, kwani shani yake ni ya ajabu mno. Angetokea wapi binadamu bilaidhini yake? Oksijeni inayotupa jeuri ya kutamba kwenye sayari hii tungeitoa wapi? Hayo ni maswali ambayo majibu yake hata mtoto wa chekechea anaweza
kuyatoa.
Utukufu
wa Mungu ndiyo kila kitu, uwezo wake ndiyo unaofanya maisha yetu yasonge mbele,hivyo hatuna budi kumhimidi, kufuata yale anayoyaamrisha na kuachana na
anayokataza ili tuzidi kujisafisha mbele yake.

Jana kwa ndugu Wakristo ilikuwa ni sherehe ya Ufufuo wa Yesu wa Nazareti.

Mapenzi yanaumiza, ndiyo maana watu wanalia! Wanateseka na machozi yanawatoka, lakini
bado wamo. Kwanini hawataki kuyaacha? Jibu la swali hili ni kitendawili
kilichojaa utata katika kukitegua.

Ni vijimambo tu vya ‘malove dave’, si unajua bila mapenzi maisha yanakuwa na
mushkeli? Bila shaka jibu ni ndiyo na huo ndiyo ukweli, binadamu hawezi kuishi
kama jiwe, mti au amoeba.

Raha ya maisha ni kuwa na mwenzi wa kumpenda na kukupenda kiukweli wala siyo
kuzugana. Hayakuumbwa mapenzi bila sisi, na hiyo ndiyo sababu ya kutangulia
Adam na Hawa kisha yenyewe yakafuata katikati yao.

Kwa wale walio katika mapenzi matamu na ya kweli watakubaliana na mimi kuwa pale penye amani ni kama paradiso ndogo ndani ya ulimwengu huu mkubwa uliojaa vituko!

Si ajabu kujikuta umeshiba bila kula, eti kwa sababu tu umemuona mpenzio au kuwa
naye karibu. Yeye si ndiye mambo yote, kwahiyo kuna haja gani ya kujaza tumbo
kwa sembe wakati sura na harufu yake vinakushibisha? Raha iliyoje!

Wakati watu wengine wakiishi kwa raha katika maisha yao ya kimapenzi, wapo wanaoteseka
huku mioyo yao ikiwa imesinyaa! Kila
siku ni karaha na vituko vya makusudi.

Japo wanawapenda sana na kuonesha mapenzi yao yote, lakini wanatendwa. Kila siku mioyo imejikunja kwa simanzi inayotokana
na maumivu yasiyojulikana mwisho wake.

Kisa kupenda!
Lakini pamoja na karaha, vituko na dharau bado kuna wale wenzangu na mimi
utakaowasikia wakisema; “Ah! Nitavumilia tu, labda atabadilika na nafikiri
sitoweza kumuacha kwa kuwa nampenda sana!”

Hey! Shtuka ndugu yangu, labda pengine mimi nikawa na msimamo tofauti kidogo.
Ninavyoamini ni kwamba mapenzi ya kweli ni pamoja na kumsikiliza mwenzako na
kuheshimu hisia zake.

Tofauti na hapo, tabia ya kutokuwa msikivu, kutojali na kutokuwa mwepesi kubadilika ni
dalili tosha ya kutokuwepo kwa upendo wa dhati. Mapenzi ni kupenda, kupendwa,
kusikilizana na kuheshimiana na si zaidi au chini ya hapo!

Kama unamkemea kuhusu tabia yake ya kurudi nyumbani usiku na hataki kubadilika,
unangoja nini tena? Hapa naomba niwape pole wale wote wanaokwazwa na wapenzi
wao kwa namna moja au nyingine.

ANGALIZO; Kama mpenzi wako anakuumiza kutokana na ulevi wake, ujeuri, kutojali, ubabe na mengineyo mengi, huo ni mtihani mzito!

Pamoja na hivyo, nafahamu kuwa wakati mwingine ni vigumu kuamua hatma ya uhusiano wako
kwakuwa unahisi unampenda sana na hauko tayari kumkosa maishani. 

don`t cry about love again


No comments: