Msanii
wa mitindo Jocktan Cosmas Maluli maarufu kama Makeke (katikati) akiwa
katika moja ya majukwaa ya fashion la Slum fashion Africa lililofanyika
nchini Kenya.
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Makeke
ni msanii wa mitindo ambaye anafanya mitindo ya kiafrika/kiasili
kutokana na maisha ya Muafrika halisi, Jina kamili ni Jocktan Cosmas
Maluli amabaye pia ni mmiliki wa kampuni ya MAKEKE AFRIKA CO.LTD
iliyopo Boko – Dar es salaam ambayo ilianzishwa mapema mwaka Desemba
2012.
Mpaka
sasa jina la MAKEKE limeweza kutumika kama jina na brand ya kibiashara
inayomtambulisha Jocktan Maluli ambaye hadi sasa ofisi yake hiyo
ikiweza kufikisha umri wa zaidi ya miaka 5 huku ikiwa na idara tatu
muhimu amabazo ni MAKEKE AFRIKA KOLEKSHENI, MAKEKE MEDIA &
MAKEKEMODELING AGENCY.
Makeke
anabainisha kuwa, alikuwa na kipaji cha uchoraji tangu akiwa mdogo, na
alishawahi kuwa mchoraji bora wa shule ya msingi wakati huo akiwa
Mbeya. Kipaji hicho aliendelea nacho na hata kidato cha nne na kidato
cha sita alipoibuka kuwa mchoraji bora wa katuni Nyanda za juu kusini na
Tanzania kwa ujumla.
Moja ya mitindo inayobuniwa na msanii wa mitindo nchini, Makeke.
Katika
uchoraji bora huo aliwahi kuzawadiwa kiasi cha pesa na cheti na
taasisi ya kuzuia rrushwa TAKUKURU, wakati huo akiwa kidato cha tano na
cha sita ndipo alipoanza kufanya mitindo kama ‘Model’ na akafanikiwa
kuwa Mr. Mbalizi high school wakati huo na Mr. Mbeya vijijini hapo ndipo
alipopewa jina la ‘Model Makeke’ kutokana na miondoko yake jukwaani,
baadae alianza kushauriwa na watu kuwa kutokana na uwezo mkubwa wa
kuchora anaweza kuwa mbunifu mzuri wa mavazi basi toka hapo ndo akaanza
rasmi ubunifu wa na watu walikuwa wakikubali kazi zake.
Baadae
akafanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha Dododma (UDOM) ambapo alikuwa
akisomea Shahada ya (FINE ARTS & DESIGN) na hapo ndipo haswa
alipotimiza ndoto zake za kuwa msanii bora wa mitindo, baadae akajiunga
na AFRIKA SANA chini ya mbunifu Alilnda Sawe kwa ajili ya mazoezi ya
vitendo.
Makeke
katika kufikia malengo yake ameweza kutimiza ndoto yake huku akiwa
Mbunifu wa nguo, ubunifu wa mapambo ya ndani pamoja na kupamba kuta,
graphics design, make up design.
Mitindo inayobuniwa na Msanii wa mitindo nchini, Makeke.
Anabainisha
kuwa, na uwezo wote huo: “Ni kwa sababu toka nikiwa mdogo nilikuwa
katika mazingira hayo ya kujifunza vitu vingi, na pia chuo kikuu
tulikuwa tukisoma aina mbali mbali za sanaa”. Anabainisha Makeke.
Anaongeza
kuwa: “Kikubwa nafkiri watu bado hawajaelewa vile mimi nafanya mambo
yangu, na pia hawajaelewa hichi kitu nnachokiita sanaa ya nguo, kiukweli
sipendi kuitwa ‘Designer’ napenda mtu aniite ‘artist’, kwa hiyo ‘Am a
fashion artist’ nafanya kitu kwa uwezo zaidi ya ule wa ‘Designer’,
sababu ‘designers’ wengi wamekuwa watu wa ku copy na ku pest (bandika
bandua) yaani hawaumizi kichwa
katika
kufanya michoro yao, mimi sina mipaka katika kufanya nguo naweza
tengeneza nguo katika mazingira yoyote kwa material yeyote. Pia watu
bado hawajanielewa kwasababu nafanya mitindo migumu ingekuwa ni muziki
basi ni muziki wa Tamaduni (Culture music) nguo nyingi si rahisi
kuvalika mtaani.” Anaeleza Makeke.
Akifafanua
juu ya tasnia ya mavazi pamoja na soko lake: Makeke anabainisha kuwa,
Tasnia ya mitindo Tanzania iko katika matabaka ambapo anabainisha
kuwa, Wapo wanamitindo wanaojiona kama miungu watu na wabinafsi hali
ambayo wanarudisha nyumba tasnia nzima ya mitindo hapa nchini.
“Mimi
sipendi mambo ya majigambo na ubinafsi. kitu ambacho sikipendi na ndio
maana niko mbali na watu wa tabia hiyo na hii ndo sababu ya kwenda
kufanyia mitindo nje ya Tanzania mara kwa mara. Huko nje watu wako
makini na wanakuelewa nini unafanya kuliko hapa nyumbani” anaeleza.
Makeke
kutokana na kufanya kazi zake nyingi nje ya Tanzania vyombo vingi vya
habari vya ndani vimekuwa vikishindwa kumpa nafasi huku vingi
vikiangalia watu waliokwisha toka na kujulikana zaidi. Kwa hali hiyo
licha ya kuwa ni mchanga katika tasnia ya mitindo anaamini sasa ni zamu
yake na Tanzania sasa inamuhitaji.
Makeke
mbali na kufanya ubunifu wa mavazi, . nje ya ubunifu anafanya: Mambo
ya upakaji rangi kuta, uchoraji wa katuni, Upigaji wa picha za matukio
na kuziwekea ubunifu zaidi, kubuni vitu ikiwemo logo, matangazo ya
mabango na vitu mbalimbali kwani anaamini hivyo vyote vinazama kwenye
sanaa , na hii ndo maana ya kuitwa msanii kutokana na kuwa navyo tokea
utoto wake na pia kuvisomea ngazi ya chuo kikuu.
Makeke
anaamini kuwa yeye yupo tofauti zaidi na wengine: “Tofauti kubwa ni
kitu kimoja nakiita CREATIVE& ARTISTIC MINDS, nna uwezo wa kubuni na
pia nna chembe chembe za kisanii ndani yangu ndio maana hata kazi zetu
hazifanani. Hata siku moja kazi yangu huwezi kukuta inafanana na mtu
mwingine hasa wabunifu hawa wa hapa nyumbani” anaeleza.
Pia
anaongeza kuwa, tofauti nyingine baina yake na wabunfu wengine ni
kwamba wao wanafanya mitindo kama kazi ya ziada lakini kwa yeye ni kazi
ya kwanza na anaifanya kama mbobezi huku akiifanya kazi hiyo ya ubunifu
kwa nyakati za sasa na baadae akimaanisha kuwa anamalengo ya mbali.
Hata
hivyo, katika ubunifu wake wa mavazi, Makeke anaweka wazi kuwa,
amekuwa akibuni kutokana na maisha ya muafrika huku hasira na ndoto
zake kubwa ni kuona mavazi ya ubunifu yanabuniwa na kutoka na yenye
kuendana na msimu wowote ule. Makeke kwa sasa ana bidhaa sokoni
‘BUTTERFLY BRAND’.
Kiwango
cha elimu yake na mwaka: Kidato cha nne (O level 2003 – 2006), Kidato
cha tano na sita (Advance. 2007 -2009) elimu hiyo ya vidato vyote akiwa
ameipatia katika shule ya Mbalizi High School iliyopo Mbeya Vijijini
Mkoani Mbeya. Makeke emezaliwa 18 Feb 1990).
Miongoni mwa kazi alizofanya kwenye majukwaa makubwa ya ubunifu na mitindo:
Majukwaa
ya ndani ni pamoja na Mbeya Redds Nait, In forest fashion show-Mikumi,
RRM fashion week, Marahaba fashion show, Lady in Red, Bagamoyo
international festival of arts and culture (2014 na 2015). Pia Makeke
ni “Official dresser miss IFM 2013, 2014, and 2015”
Robi-
Slum Fashion Africa, Kisumu Fashion Week, Fashion & Style Expo-
Nairobi. The Designer walk ( Kenya) fashion show – TDWFS – (Afrika
Kusini).
Kwa
majukwaa ya nje ya Tanzania (International) ni pamoja na : Slum
fashion Africa, Picha fashion Festival, The designers walk fashion show,
The reality tv fashion show, East African motor show.
Majukwaa
mengine anayotarajia kupanda hapo baaadae: Bongo style competition,
East Africa Fashion week, Ekhulen fashion show based on SADC countries
members, Abuja International Fashion.
Watu
walio kwenye tasnia ya Ubunifu wanaomvutia ni pamoja na : Henrick
Biscouvs (Scandnavia),Ken Kasea (Morogoro), Kipilyango wa Africa
shiners Tz, Ailinda Sawe (Tanzania) na Asia Idorous.
Miongoni mwa ubunifu na mitindoanayotamba nayo, Makeke.
Baadhi ya mitindo ya ubunifu ya Makeke.
mitindo hiyo anayobuni Makeke.
Msanii wa mitindo, Makeke akiwa katika moja ya mitindo yake..
No comments:
Post a Comment