Mbunge
wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulya (CUF) (katikati) akiwa pamoja na
wanasheria wanaosimamia kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa kwa wakazi
wa mabondeni waliopo kweny mabonde ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Awali 14 Januari mwaka huu Mahakama Kuu ya Ardhi ilisogeza mbele
usikilizwaji wa kesi ya msingi ya kupinga kubomolewa kwa nyumba za
Mabondeni hasa zile zilizopo kwenye bonde la jimbo hilo la Kinondoni.
Hata
hivyo inaelezwa kuwa leo inaweza hali ikawa tofauti kwa wananchi wa
mabondeni wanaofika kusikilizwa kesi yao kwani jibu lolote litakalotoka
litakuwa mwiba kwao na kufanya hali kuwa ngumu kwa upande huo wa
wananchi ambao jicho na sikio lao wakilielekeza kwa Mbunge wao pamoja na
Mawakili wanaosikiliza kesi.
“Wanasema
mbichi mbivu basi kujulikana mchana wa leo 25 Januari. Maamuzi ya
Mahakama Kuu ya Ardhi itakayoyatoa ndio mwisho wa utata na hali halisi
ya tukio linaloendelea sasa” kilieleza chanzo kutoka kwa watu
waliokwenye kamati ya kushughulikia kesi hiyo wanaoishi mabondeni.
Hata
hivyo mbichi na mbivu ni kwa wakazi hao wa mabondeni ambao licha ya
waliobomolewa, pia wapo ambao nyumba zao zimewekewa alama ya X
wakitakiwa kuzibomoa maramoja huku wengine wakiwa na wasiwasi ya
kubomolewa baada a kutoelewa kama wapo bondeni ama sehemu ambayo
hairuhusiwi kwa shughuli za makazi.
No comments:
Post a Comment