Mwezi mmoja toka mauaji ya Baga Nigeria - LEKULE

Breaking

3 Feb 2015

Mwezi mmoja toka mauaji ya Baga Nigeria

Mji wa Baga ulioshambuliwa na Boko Haram 


Leo ni mwezi mmoja tangu wapiganaji wa Boko Haram waliposhambulia miji ya Baga na Doron Baga kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Idadi kamili ya watu waliokufa haijulikani lakini inadaiwa kuwa ni kati ya watu mia moja na hamsini hadi elfu mbili.

Wakati wapiganaji wa Boko Haram wakivamia kutoka upande wa magharibi wa Baga, kundi la vijana waliodhamiria kupambana na kundi hili walijaribu kuulinda mji wao.

Yalikuwa mafanikio ya nadra kutokea dhidi ya Boko Haram. Kulikuwa na ahueni lakini haikudumu muda mrefu.

Ilikuwa taharuki. Wanawake na watoto, vijana na wazee walizikimbia nyumba zao na biashara, wengi wakikimbilia mji jirani wa uvuvi wa Doron Baga ulio ufukweni mwa Ziwa Chad.Boko Haram waliwafuata Doron.

Iwapo bunduki haikukudhuru, walianza kuua watu kwa kuwagonga na magari yao. Ufyatuaji wa risasi haukuchagua pa kulenga

Mauaji ya Baga na Doron Baga yalitokea mwezi mmoja uliopita…Boko Haram hawakusambaratishwa. Tangu wakati huo, waasi hao wameishambulia miji mingi zaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria; watu wengi wamekufa na wengi zaidi wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

No comments: