Mahabusu mmoja Shabani Ramadhani (28), amekutwa amejinyonga katika choo cha Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki, jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea jana baada ya mahabusu huyo kufikishwa katika kituo hicho juzi akituhumiwa kufanya tukio la unyang’anyi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Augustino Senga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu alijinyonga kwa kutumia kamba ya kaptura aliyovaa.
Kamanda Senga alisema marehemu alijinyonga alfajiri katika choo wanachokitumia mahabusu hao na mwili wake kugundulika nusu saa baadaye.
“Alikwenda chooni kati ya majira ya saa tisa na saa kumi alfajiri wakati wenzake wakiwa wamelala na ndiko alikojinyongea kwa kutumia kamba ya kaptura yake, lakini uchunguzi unaendelea,” alisema Senga.
Mama mdogo wa marehemu ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema kuwa Ramadhani alikamatwa na Polisi Ijumaa iliyopita na kufikishwa katika kituo hicho akiwa salama.
Alisema jana walifika katika kituo hicho kwa ajili ya taratibu za kumwekea dhamana, ndipo walipoelezwa kuwa ndugu yao amefariki dunia kwa kujinyonga na kamba.
“Sisi wenyewe tunashangaa iweje kajinyonga wakati tunavyofahamu mtuhumiwa anapofikishwa polisi anatolewa vitu vyote alivyonavyo na kuingizwa mahabusu?,” alihoji mama huy
No comments:
Post a Comment