Msafara wa jeshi washambuliwa Mali - LEKULE

26 Jan 2015

Msafara wa jeshi washambuliwa Mali


 Ripoti kutoka nchini Mali zinasema kuwa watu wasiojulikana wameshambulia msafara wa kijeshi karibu na mji wa Timbuktu.
Wanajeshi wawili waliuawa kwenye mji ulio kaskazini wa Douékiré.
Shambuliz hilo linajiri wakati ambapo kiwango cha mashambulizi kimeongezeka siku za hivi majuzi.
Wiki iliyopita watu waliokuwa na silaha waliishambulia kambi moja ya umoja wa mataifa na kumuua mlinda amani mmoja kutoka Chad.

No comments: