Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa leo anatarajia kuanza ziara ya siku 14 katika mikoa ya Kanda Ziwa kukagua shughuli na miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema Waziri Mkuu anayetarajiwa kufika Mwanza saa nane mchana, atatembelea mikoa ya Simiyu, Kigoma, Geita na Kagera.
“Ingawa hakuna ratiba ya kutembelea eneo lolote mkoani Mwanza, tumejipanga kila idara endapo atafanya ziara ya kushtukiza, tuko tayari,” alisema.
Wakati huohuo; Mulongo alisema mke wa Rais, Janet Magufuli anatarajiwa kutembelea Kituo cha Kulea Wazee Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi.
“Ziara hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8, kila mwaka,” alisema Mulongo.
No comments:
Post a Comment