Mkufunzi wa kilabu ya Liverpool Jurgen Klopp atakutana na timu yake ya
zamani Borussia Dortmund katika robofanili ya kombe la Europa.
Klopp mwenye umri wa miaka 48 aliondoka Dortmund msimu uliopita baada ya
kuiongoza timu hiyo shinda mataji mawili ya Bundesliga na kufika katika
fainali ya vilabu bingwa Ulaya.
Sevilla,ambayo inajribu kushinda kombe hilo kwa mara ya tatu
itakabiliana na Athelitico Bilbao katika mechi inayoshirikisha timu zote
za Uhispania.
Villareal pia kutoka ligi ya Uhispania itachuana na timu ya Czech Sparta
Prague huku kilabu ya Ureno Braga ikikabiliana na Shakhtar Donetsk
kutoka Ukraine.
Mechi hizo za robo fainali zitachezwa mnamo tarehe 7 na 14 mwezi Aprili.
Liverpool itasafiri Dortmund katika awamu ya kwanza ya mechi.
No comments:
Post a Comment