Msanii
Ray C amevijia juu vyombo vya habari vinavyoandika taarifa za uongo juu
yake, kuwa amerudia kutumia madawa ya kulevya, na kuahidi safari hii
atavifikisha mahakamani.
Katika
ukurasa wake wa instagrama Ray C ameandika ujumbe mrefu kuhusu vyombo
vya habari vinavyomchafua, na kwamba wana mpango wa kukwamisha harakati
zake za kupambana na madawa ya kulevya.
“Hujuma
hizi najua mnazifanya ili niishie njiani katika harakati za kupambana
na dawa za kulevya nchini, Mimi na taasis yangu nitaendelea kusonga
mbele na hakika sitakwamishwa na nyumbu kama hawa kwanza mwonekano wa
picha uko wazi mimi sina nywele fupi kiasi hicho Ray C wa sasa si yule
wa kipindi na enzi hizo now I'm not catalysts of drugs, hata hivyo
tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu ili niweze kuwawajibisha hawa
nyumbu” aliandika Ray C.
Pia
Ray c amesema kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya mwisho kuandaa nyimbo
yake, japokuwa bado yuko kwenye dozi ya methadone, inayotibu uathirika
wa madawa ya kulevya.
“Mimi Niko katika maandalizi yangu ya mwisho ya kuaanda nyimbo yangu japo bado niko katika dose ya methadone”, aliandika Ray c.
No comments:
Post a Comment