Wakati
Ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga
ukitarajiwa kuanza baada ya hatua mbalimbali za mazungumzo kukamilika,
taarifa zilizotoka March 28 2016 ni kwamba huu mradi umeziingiza
Tanzania na Kenya kwenye mvutano.
Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini Prof Justin Ntalikwa amekiri kuwepo kwa mvutano ila ametoa uhakika wa asilimia 98 kwa Tanzania kuuchuka mradi huo >>>’kwanza
tuna uzoefu mkubwa katika ujenzi wa haya mabomba, tuna mabomba kama
manne hivi ambayo tayari tumeshayajenga, uwepo wa bandari ya kina kirefu
iliyopo Tanga ambayo inaweza kuchukua meli mbalimbali ambazo zinakuja
kuchukua hayo mafuta, vilevile nchi yetu ina usalama zaidi
ikilinganishwa na hao wenzetu tunaoshindana nao’
Kingine
alichothibitisha ni kwamba wamekutana na wafanyabiashara ili kujadili ni
jinsi gani wafanyabiashara hao wanaweza kuchangia katika kuchukua fursa
mbalimbali zitakazojitokeza baada ya kuupata mradi wa ujenzi wa bomba
la mafuta ghafi unaotarajiwa kujengwa.
>>>‘kwenye
huo mradi kuna fursa ambazo ni pamoja na kupata tenda mbalimbali katika
kazi zitakazojitokeza, ajira zitakazoweza kupatikana kwa ajili ya watu
wetu Tanzania na pia kuna kodi mbalimbali zitapatikana kwa kulipwa
kupitia huo mradi
No comments:
Post a Comment