Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kwa Mamlaka
aliyopewa amemteua Profesa MAYUNGA HABIBU NKUNYA kuwa Mwenyekiti wa Bodi
ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kuanzia Februari 17, 2016.
Uteuzi huo ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 17 Februari, 2016 hadi 16 Februari, 2019.
Kabla ya
uteuzi huo Profesa Nkunya alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya
Programu ya Mapitio ya Mfumo wa Taifa wa Ubunifu (National Innovation
System Review Programme).
Uteuzi huo unafuatia kumalizika kwa muda wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Taarifa hii imetolewa na,
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI),
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
01 Machi, 2016
No comments:
Post a Comment