Al Shabab yawaua 24 wakitizama Man U-Arsenal
Watu 24
wameuawa mjini Baidoa Kusini mwa Somalia wakitizama mechi baina ya
Manchester United na Arsenal baada ya shambulizi lililotekelezwa na Al
Shabab.
Taarifa
za awali zinaeleza kuwa milipuko miwili mikubwa ilitokea, katika mkahawa
huo uliokuwa umejaa mashabiki wa mechi kati ya Manchester United na
Arsenal.
Miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na afisa wa serikali ya jiji hilo.
Mji wa Baidoa ulitekwa na wapiganaji waislamu wa Al-Shabaab mwaka wa 2008, lakini walitimuliwa mwaka 2012.
Mji huo
ulioko takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu ni mji wa hivi
punde zaidi kushambuliwa na wanamgambo hao wa kiislamu.
Shambulizi
la kwanza lilitokea katika mgahawa maarufu unaopendwa na wageni na
viongozi wa kisiasa ambao ulishambuliwa kwa gari lililokuwa limetegwa
bomu.
Walionusurika waliokolewa na wanajeshi wa muungano wa Afrika AMISOM.
Shambulizi
hili limetokea muda mchache tu baada ya kukamilika kwa warsha ya
viongozi wa mataifa yanayochangia wanajeshi wake katika jeshi la
muungano wa Afrika AMISOM.
Siku ya ijumaa watu wengine zaidi ya 20 waliuawa katika mgahawa mwengine kufuatia shambulizi la Al Shabaab.BBC
No comments:
Post a Comment