Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajia kuwa mgeni
rasmi kwenye Tamasha la Pasaka jijini Mwanza Machi 27.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex
Msama Waziri Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo
litaanzia Geita Machi 26 na kumalizia Kahama Machi 28.
Msama
alisema kamati yake inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha hilo
ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.
“Maandalizi
kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya
Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi
wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.
Msama
alisema baadhi ya waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ambao
ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM
Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher
Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro na Kwaya ya Wakorintho Wapili.
Aidha Msama alisema viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na kwa watoto shilingi 2000.
No comments:
Post a Comment