Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, aliyeapishwa jana kushika wadhifa huo na Rais Dk. John Magufuli, amefunguka na kueleza sababu za kuitwa Waziri ‘mzigo’ wakati akiwa Wizara ya Maji, akitokea Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Novemba
24,mwaka 2013, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman
Kinana, akiwa kwenye ziara za kuimarisha na kukagua Ilani ya chama hicho
mkoani Ruvuma, kabla ya kuanza kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,
alikutana na malalamiko ya wananchi juu ya uzembe wa mawaziri waliokuwa
kwenye Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, waliowaita ‘mizigo’.
Mawaziri
wengine waliotajwa kuwa mizigo ni Dk. Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi), Christropher Chiza (Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika) na Naibu wake
Akijibu
tuhuma hizo baada ya kupenya kwenye Baraza la Mawaziri la Rais Dk.
Magufuli, tofauti na watu wengi walivyodhani kutokana kashfa hiyo,
Profesa Maghembe alisema waliomtaja kuwa ni mzigo ni majangili waliokuwa
wanawinda wanyama na waandishi waliokuwa wanaandika na kulipwa na
majangili.
“Wanaosema
Waziri Maghembe ni mzigo hawajui na hawajafanya utafiti na usipofanya
utafiti, huna haki ya kuzungumza, na wafikishieni taarifa Maghembe
amerudi tena,” alisema.
Alisema amejipanga kuhakikisha anapambana na ujangili nchini na kuongeza pato la taifa kupitia sekta hiyo.
Alisema amejipanga kuhakikisha anapambana na ujangili nchini na kuongeza pato la taifa kupitia sekta hiyo.
Alisema atahakikisha wizara hiyo inaenda vizuri na rasilimali zilizopo zinalindwa ili zilifaidishe taifa.
“Jambo la kwanza nitakalolifanya ni kupambana na ujangili na
tunawatumia salamu majangili wote kokote walipo, kiama chao kimefika…kwa
sasa wakae nyumbani watafute shughuli za kufanya,” alisema.
Alitaja jambo la pili atakalolifanya katika sekta hiyo ni
kuhakikisha misitu inatunzwa na kudhibiti watu wote wanaokata miti na
kuchoma mkaa.
“Tutahakikisha mkaa utakaokuwa unachomwa ni ule wa lazima na siyo
kuchoma hovyo. Hivyo tutaangalia namna ya kurahisisha nishati zilizopo
ili kupunguza matumizi ya mkaa,” alisema.
Prof. Magembe alisema jambo la tatu ni kuhamasisha utalii na
kuongeza idadi ya watalii kutoka nje kutoka milioni 1.2 hadi kufikia
milioni tatu katika kipindi cha miaka mitatu.
“Hii ni sekta muhimu na ili kuongeza idadi ya watalii kufikia
milioni mbili hadi tatu kwa kipindi cha miaka miwili ama mitatu ijayo ni
lazima kuhamasisha,”alisema.
Alisema
mwaka 2007 akiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, katika kipindi hicho,
alifanya kazi kubwa ya kuhakikisha katika sekta ya uwindaji wanaongeza
mapato ya serikali kuanzia Dola milioni saba zilizokuwa zinapatikana
hadi kufikia Dola milioni 70 na kwa msingi huo, yeye siyo mzigo.
Alisema
pia walikuwa wakifanya kazi ya kukamata watu wanaosafirisha magogo
kwenda nje ya nchi na kuongeza pato la taifa katika sekta ya misitu.
“Nashangaa hawa wanaoniita mimi ni mzigo, ningewezaje kufanya kazi hizi,” alisema Profesa Maghembe.
No comments:
Post a Comment