Inspekta
Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu amelifumua Jeshi la Polisi
nchini kwa kupanga na kupangua vigogo wake, huku baadhi wakipandishwa
nyadhifa.
Pangapangua
hiyo imewagusa pia maofisa waandamizi wa jeshi hilo walioko makao
makuu, makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa (RCO) na wakuu wa
polisi wa wilaya (OCD).
Habari
za uhakika kutoka ndani ya makao makuu ya Jeshi la Polisi zinasema
pangapangua hiyo imewagusa pia wakuu wa vikosi, wakuu wa polisi wa vituo
(OCS) na polisi wa vyeo cha chini.
Akizungumza jana, msemaji wa polisi, Advera Bulimba alisema: “Mabadiliko hayo ni ya kawaida ya ndani, hayana uhusiano na kasi ya Rais John Magufuli ila kazi lazima ifanyike.”
Mabadiliko
hayo yamekuja ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kukutana na maofisa wa polisi kwenye Bwalo la Maofisa wa jeshi hilo
Oysterbay jijini Dar es Salaam na kati ya mambo yaliyotajwa ni
kukumbushana utendaji, uwajibikaji na mpango wa kulifumua jeshi hilo.
Chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi kimedokeza kuwa orodha ya waliokumbwa na pangapangua hiyo ni ndefu .
“Nafikiri
IGP ameamua kusuka upya safu ya uongozi ili kuboresha ufanisi katika
utendaji wa kazi. Unajua jeshi lazima liendane na falsafa ya Rais
Magufuli (John) ya Hapa Kazi Tu,” alidokeza afisa mwingine.
Mabadiliko
hayo yamekuja wakati tayari makamanda wa polisi wa baadhi ya mikoa
wakiwa wamebadilishwa katika vitengo walivyokuwa awali, wakiwamo Kikosi
cha Usalama Barabarani, ili kuboresha utendaji wa jeshi hilo.
Katika
mabadiliko hayo, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP), Salehe Ambika
amehamishwa kutoka kitengo cha Sheria na Huduma za Utafiti kwenda kuwa
mkuu wa utawala.
DCP
Robert Boaz amehamishwa kutoka kitengo cha intelijensia kwenda kuwa
mkuu wa kitengo cha uhalifu wa kitaifa na uhalifu wa kupangwa au
Transnational and Organized Crime (TOC).
Katika
panguapangua hiyo, Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Luteta Modest
amehamishwa kutoka kitengo cha sheria kwenda kuwa mkuu wa kitengo cha
sheria na huduma za utafiti.
Mkoa
wa Kilimanjaro umetikiswa zaidi na mabadiliko hayo baada ya maofisa
watano waandamizi kuhamishiwa vituo vipya na nafasi zao kuchukuliwa na
sura mpya.
Kamanda
wa polisi wa mkoa huo, Fulgence Ngonyani amehamishiwa Chuo cha Polisi
Kilwa Road, na RCO Ramadhan Ng’anzi amehamishiwa mkoa wa Shinyanga
kuendelea na wadhifa huo.
OCD
wa Moshi, Mrakibu Mwandamizi Deusdedit Kasindo amepanda cheo na kwenda
kuwa kamanda wa Mtwara, wakati mkuu wa kitengo cha FFU wa mkoa huo,
amehamishiwa mkoa mwingine.
Katika
mabadiliko hayo, kamanda wa mkoa wa Iringa, Kamishina Msaidizi Ramadhan
Mungi amehamishiwa Kilimanjaro kuchukua nafasi ya Ngonyani anayekwenda
chuoni.
Nafasi ya RCO wa Kilimanjaro imechukuliwa na SSP Black Magesa aliyekuwa OCD Korogwe.
Kamanda
wa Mkoa wa Manyara, ACP Christopher Fuime amehamishiwa Kinondoni
kuendelea na wadhifa huo, wakati kamanda wa Ruvuma, ACP Mihayo Miskhela
amehamishiwa mkoani Tanga.
Pia,
kamanda wa Mkoa wa Tanga, ACP Zuneri Mumbeki amehamishiwa Ruvuma
kuendelea na wadhifa huo, huku kamanda wa Kinondoni, SP Camilius Wambura
amehamishiwa Mkoa wa Manyara kushika wadhifa huo.
Maofisa
wengine ni Gerald Ngichi, ambaye alikuwa OCD Magomeni, amehamishiwa
Lindi, Nsekela M. Nsekela (OCD Nyang’wale sasa ofisa mnadhimu II Rorya,
Nesto Msembele (OCD Mbalizi sasa Polisi Jamii Mbeya), William Malei
(ofisa mnadhimu ll Kigoma, sasa OCD Korogwe), Melard Sindano (OCD
Kigoma, sasa OCD Nyang’wale).
Wengine
ni Patrilinius Mlowe (OC-CID Kwimba, sasa OCD Kawe, Edson Kasekwa (OCD
Makambako, sasa OCD Kilolo), Agustino Titus (mnadhimu ll Morogoro, sasa
OCS Malinyi).
Katika
pangua pangua hiyo, Raphael Msela (ofisi ya RCO Kagera, sasa naibu RCO
Kagera), John Samwel (OCS Malinyi, sasa ofisa mnadhimu II Morogoro), SP
Debora Mrema (polisi jamii Mbeya, sasa OCD Mbalizi, SP Omari Mtungu (OCD
Tanga, sasa OCD Moshi),SP Alfred Mwaikusa ambaye alikuwa OCS Singida
sasa anakwenda kuwa OC-CID Serengeti.
Wengine
ni SP Limited Mhongole ambaye alikuwa OC-CID Mbarali sasa anakuwa OCD
Mbarali, ACP Jaffar Mohamed (RPC Pwani, sasa makao makuu) na ACP Peter
Kakamba anakuwa RPC Iringa.
Pia
ACP Mussa Taibu aliyekuwa RCO Shinyanga, sasa anapelekwa upelelezi
makao makuu, SSP Pili Omari (OCD Kawe, sasa OCD Mwanga, David Chidingi
(OCD Lindi, sasa OCD Magomeni, SSP Constantiono Mbugambi (OCD Mwanga,
sasa OCD Ngara), SSP Jullius Lukindo (OCD Mbarali, sasa OCD
Mvomero).
No comments:
Post a Comment