Serikali
ya awamu ya tano imeshauriwa kuendelea na adhma yake ya kudhibiti
watumishi wa umma wanaotumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi.
Katika
kuadhimisha sikukuu ya Krisimas mkoani Morogoro Askofu mkuu wa kanisa
la KKKT Dayosisi ya Morogoro Askofu Jackob Mameo ameiomba serikali
kuendelea na msimamo wake wa kuwawajibisha watumishi wanaotumia nafasi
zao kwa manufaa binafsi ili wananchi hasa wanaoishi vijijini wanufaike
na rasilimali za taifa lao.
Akiongoza
ibada ya misa ya sikukuu ya Krismas Askofu Mameo amepongeza juhudi za
serikali ya awamu ya tano ambapo amesema asilimia kubwa ya wananchi wa
vijijini wanaishi katika mazingira magumu kwa kukosa huduma muhimu za
maji, umeme pamoja na miundombinu bora ya barabara…
kwa
upande wao waumini wa kikristo wameomba vyombo vya ulinzi kuhakikisha
wanalinda usalama katika maeneo yote yenye mkusanyiko wa watu ili
kuepusha uvunjifu wa amani unaoweza kujitokeza ambapo pia wamewataka
watanzania kusherekea sikukuu hii ya krismas kwa amani na utulivu bila
kubaguana
No comments:
Post a Comment