Ridhiwan Kikwete Alikana Gazeti La Mawio.......Adai aliyekuwa Anamsaidia Kufunga Viatu Sio Paul Makonda,Ni Deogratias Kessy - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 25 December 2015

Ridhiwan Kikwete Alikana Gazeti La Mawio.......Adai aliyekuwa Anamsaidia Kufunga Viatu Sio Paul Makonda,Ni Deogratias Kessy


Mbunge wa Chalinze, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amekanusha aliyekuwa anamsaidia kufunga kamba za viatu katika picha iliyochapishwa kwenye gazeti la MAWIO (picha juu) si Paul Makonda Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na waandishi wa habari , Ridhiwani Kikwete alisema anayeonekana akimsaidia kufunga viatu katika picha hiyo ni Deogratias Kessy, mfanyakazi katika kampuni ya ushonaji na mavazi ya Sheria Ngowi.

"Nilishona safari suti katika kampuni hiyo. Nilipokwenda kuchukua nguo yangu na nilipovaa ili kuona kama imeshonwa vizuri, Bwana Sheria Ngowi akanitaka nivae viatu vya ngozi.

"Bahati mbaya nilikuwa nimevaa sandals hivyo akaamua kunipa viatu vya dukani kwake nivae. Wakati Bwana Deogratias akinisaidia kuvaa viatu ndipo mpiga picha wa kampuni ya Sheria Ngowi akapiga picha hiyo kwa matumizi yao. Nashangaa kuona watu wanaitumia picha hiyo kwa makusudi yao yasiyo sahihi," alisema Ridhiwani Kikwete.

Sielewi kwanini waandishi wa habari wa MAWIO wanaamua kuandika taarifa za uzushi. MAWIO walikuwa na nafasi ya kuniuliza au kwenda kwa Sheria Ngowi kujua ukweli wa wanachoandika.


Ridhiwani alitahadharisha kuhusu vyombo vya habari kutumika kwa malengo ya kuwachafua watu.
Post a Comment