Ndege ya shirika moja la ndege la urusi,iliyokuwa na abiria zaidi ya mia mbili imeanguka katika eneo la Sinai nchini Misri.
Ofisi ya waziri mkuu wa misri imethibitisha ajali hiyo na kusema
ndege hiyo aina ya AIRBUS A-321 ilikuwa imetoka mji wa Sharm el-Sheikh
ikielekea mji wa SAINTT PETERSBURG nchini Urusi ilipoanguka.
Vyombo vya habari vya misri vimesema mabaki ya ndege hiyo
yamepatikana na gari ishirini za kubebea wagonjwa zimetumwa eneo la
ajali.
Awali, kulikuwepo na utata kuhusu hatima ya ndege hiyo, kwa baadhi
ya taarifa zilisema ajali hiyo ilitokea karibu na visiwa vya CYPRUS,
lakini taarifa ya afisa katika ofisi ya waziri mkuu wa misri SHARIF
ISMAIL imethibitisha kuwa ndege hiyo ilianguka katikati mwa eneo la
Sinai na kuongeza kuwa ofisi hiyo imeunda kamati ya dharura ya
kushughulikia ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment