Taasisi
ya mwalimu Nyerere imeitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufanya
kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na sheria na sio kutanguliza mbele
maslahi binafsi ya kisiasa hatua ambayo amesema inaweza kusababisha
machafukona umwagaji wa damu.
Akizungumza na vyombo vya habari mjini musoma,mmoja ya watu
aliyewahi kuwa mshauri wa baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere
Bw.Joseph Butiku,amesema amekerwa na tabia ya ZEC kusitisha uchaguzi na
kushindwa kuwatangazia wananchi kiongozi wao waliomchagua,huku
ikishindwa kuheshimu matakwa ya wananchi walipiga kura katika visiwa
vya Zanzibar.
Aidha Bw.Butiku ambaye ni kada wa chama cha mapinduzi CCM amewataka
wananchi wazanzibar kutokubali tena kurudia upigaji wa kura hadi hapo
yatakapotolewa maelezo ya kuridhisha na wahusika waliosababisha
uchaguzi huo kufutwa pia waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa sababu hiyo amewataka viongozi kuheshimu sheria na katiba ya
nchi na kwamba chama ambacho kinadhani kimeshindwa katika uchaguzi huo
kikubali matokeo badala ya kuifanya zanzibar ni mali ya chama fulani
pekeee.
No comments:
Post a Comment