Wakazi
zaidi ya 100 wa mtaa wa Kasera Kange jijini Tanga wameagizwa kuvunja
nyumba zao kisha kuondoka mara moja katika eneo hilo kufuatia baadhi ya
viongozi wa serikali kumega sehemu ya ardhi ya mwekezaji kisha kuwapatia
wananchi.
Wakizungumza na katika eneo la tukio baadhi ya waathirika
waliouziwa ardhi katika eneo hilo miaka saba iliyopita wamesema
hawatakubali kuondoka katika mazingira ya utatanishi kwa sababu viongozi
wa serikali ya mtaa wa kasera walipatiwa hati zinazowasaidia
kuwatambulisha kuwa ni wamiliki halali wa eneo hilo.
Akijibu tuhuma za kuwauzia viwanja wakazi wake na taratibu
zilizotumika kuwapatia hati miliki za serikali za mitaa,mwenyekiti wa
serikali ya mtaa wa Kasera Kange Bwana.Rajab Mbalazi amekiri kuwapatia
ardhi wakazi hao isipokuwa baada ya wakazi kuanza kuchangamkia eneo hilo
maafisa mipango miji waliwaagiza wananchi kuacha mara moja ujenzi wa
nyumba ili kuepuka kubomolewa.
Kufuatia hatua hiyo mwekezaji wa eneo hilo Bwana.Danniel Mmbaga
amesema kuwa eneo hilo wanalimiliki kisheria kwa mkataba wa miaka 99
hivyo amewaagiza wakazi hao hata kama wamejenga miundo mbinu katika eneo
hilo ni vyema wakaondoka kabla sheria haijachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment