WAFANYAKAZI
wanane wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), wanaokabiliwa na tuhuma za
kughushi vyeti vya kidato cha nne wamekutwa wana kesi ya kujibu.
Uamuzi
huo ulitolewa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupitia
ushahidi wa mashahidi wanane wa upande wa mashtaka na kuona kwamba kuna
haja kwa washtakiwa kujitetea.
Washtakiwa
katika kesi hiyo ni Justina Mungai, Christina Ntemi, Siamini Kombakono,
Janeth Mahenge, Beata Massawe, Jackline Juma, Philimina Mtagurwa na
Amina Mwinchumu.
Uamuzi
huo ulitolewa na Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba, wakati kesi hiyo
inaendeshwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro.
“Mahakama
imepitia ushahidi wa mashahidi wanane wa upande wa Jamhuri, imeuona
kwamba ushahidi huo una nguvu, hivyo washtakiwa mna kesi ya kujibu,
mnatakiwa kujitetea,” alisema Hakimu Mwaseba.
Baada ya kusema hayo mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Juni 17 na 18 mwaka huu, kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea.
Kwa
mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kughushi vyeti vya
kuhitimu kidato cha nne na kutoa hati za uongo kwa mwajiri wao ambaye
ni BoT.
Washtakiwa
Justina, Beata na Amina wanadaiwa kughushi vyeti hivyo mwaka 2001.
Christina, Siamini, Janeth na Philimina, wanadaiwa kughushi vyeti hivyo
mwaka 2002.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kughushi vyeti hivyo na kutoa hati za uongo BoT kuonyesha
vimetolewa na Baraza la Mitihani Tanzania wakati si kweli.
No comments:
Post a Comment