HUKUMU
ya kesi ya kumshambulia mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa mwaka
2010 inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe, iliyotarajiwa
kutolewa jana katika mahakama ya Wilaya ya Hai, imeahirishwa hadi Julai
17 mwaka huu baada Mbowe kushindwa kufika mahakamani.
Mbowe
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema),ilidaiwa alishindwa kufika mahakamani n kutokana na kutoa
udhuru wa kubanwa na kazi za serikali likiwamo bunge la bajeti
linaloendelea Dodoma.
Hukumu
ya kesi hiyo imeahirishwa kwa mara ya pili sasa. Kwa mara ya kwanza
hukumu ilikuwa itolewe Mei 11 mwaka huu lakini ilishindikana baada ya
Hakimu Mfawidhi, Denis Mpelembwa kuwa nje ya mahakama kwa shughuli za
ofisi.
Akiahirisha
kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mpelembwa alisema alishindwa kufika
mahakamani hapo kutokana na kubanwa na shughuli za serikali hivyo
kupangiwa siku nyingine kwa ajili ya kusomewa hukumu.
Katika
kesi hiyo ya jinai namba 73 ya mwaka 2011, Mbowe akiwa mmoja kati ya
wagombea ubunge wa Hai, mwaka 2010, anadaiwa kumshambulia Nassir
Yamin katika Kijiji cha Nshara, Kata ya Machame Kaskazini, Wilaya ya Hai
mkoani Kilimanjaro.
Katika
uchaguzi huo wa mwaka 2010, Mbowe alishinda kwa kupata kura 28,585
akifuatiwa na Fuya Kimbita (CCM) aliyepata kura 23,349, Hawa Kihogo
(UDP) kura 258 na Petro Kisimbo (TLP) 135.
No comments:
Post a Comment