ALIYEKUWA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja anatarajia kuanza
kujitetea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kwa tuhuma za
matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh
bilioni 11.7.
Washtakiwa
hao walipanda kizimbani jana mbele ya Mahakimu Wakazi Sam Rumanyika na
Saul Kinemela, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya Mgonja kuanza
kujitetea.
Mgonja
hakuweza kujitetea na kesi iliahirishwa hadi leo kutokana na Mwenyekiti
wa Jopo la Mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji John Utamwa,
kushindwa kufika mahakamani hapo.
Kwa mara ya mwisho, kesi hiyo ilipangwa kwa utetezi kuanzia jana hadi Mei 29, mwaka huu.
Mgonja
na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na Waziri wa Nishati na
Madini, Daniel Yona, wanakabiliwa na kesi hiyo, iliyoko katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mramba,
Yona na Mgonja wanakabiliwa na mashtaka 11 ya matumizi mabaya ya
madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kutokana na
kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart.
Mshtakiwa wa kwanza Mramba na wa pili Yona walikwisha kumaliza kutoa ushahidi katika kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment