SERIKALI
imewatoa hofu Watanzania wote Bara na Visiwani kuwa nchi iko salama na
inaendelea kuwa salama pamoja na kuwapo kwa vitisho kwa njia ya mtandao.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Yussuf Masauni, wakati wa kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti
Maalumu, Tauhida Nyimbo (CCM) aliyetaka kauli ya serikali kutokana
kuwapo kwa taarifa za vitisho zinazotolewa kwenye mtandao wakati huu wa
maandalizi ya sikukuu ya Idd el Fitr.
Alisema
pamoja na kuwapo kwa vitendo vya kiuhalifu vinavyotokea, nchi bado iko
salama na itaendelea kuwa salama kutokana na serikali kuhakikisha
inadhibiti uhalifu huo.
Serikali imeendelea kusisitiza kuwa mikutano ya kisiasa itaendelea kuzuiwa hadi pale polisi watakapoona inafaa kufanyika.
No comments:
Post a Comment