Ripoti ya sakata la mkataba wa kampuni ya Lugumi Enteprises na Jeshi la Polisi, ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge, sasa itawasilishwa kwenye mkutano ujao.
Makamu
mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi
alisema ripoti hiyo itaunganishwa katika taarifa za kamati ambazo kwa
utaratibu huwasilishwa kwenye mkutano huo.
Sakata
hilo linahusisha utekelezaji mbovu wa mkataba wa kufunga mashine za
kielektroniki za kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi.
Hadi
wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akifanya
ukaguzi wa mkataba huo wa Sh37 bilioni uliosainiwa mwaka 2013, ni vituo
14 tu vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, lakini mzabuni alishalipwa
Sh36 bilioni.
Baada
ya sakata hilo kuibuliwa, wabunge walitaka liwasilishwe kwenye mkutano
unaoendelea mjini Dodoma, lakini PAC ikaunda kamati ndogo ambayo sasa
inatakiwa iwasilishe ripoti ya uchunguzi wake.
Hadi jana asubuhi ripoti ya kamati hiyo ndogo, iliyoundwa na wajumbe tisa, ilikuwa bado haijawasilisha ripoti yao.
Hata
hivyo, Aeshi ambaye pia ni mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), alisema
alitarajia kukabidhiwa ripoti hiyo na kamati ndogo jana na baada ya hapo
kazi ya uchambuzi wa kamati nzima itaanza.
No comments:
Post a Comment