MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemsimamisha kazi Mhandisi wa
Mkoa, Josephat Shehemba kwa kushindwa kutimiza wajibu wake, ikiwemo
usimamizi wa barabara na kusababisha kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Makonda alisema
amefikia uamuzi wa kumsimamisha kazi baada ya kuona injinia huyo
ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya usimamizi.
Alisema
jukumu la usimamizi wa barabara, unapaswa kuwa chini ya Shehemba,
lakini ameshindwa kufanya hivyo jambo lililosababisha usimamizi huo
kufanya na wananchi na wakuu wa wilaya ambao sio kazi yao kufanya hivyo.
“Ni
lazima alitakiwa kufanya kazi yake ya usimamizi na kuhakikisha barabara
zinajengwa kwa kiwango kinachotakiwa lakini matokeo yake kazi yake
ameiacha na kufanya na watu wengine ambao hawakupaswa kufanya hivyo,” alisema Makonda.
Aidha,
Makonda alisema kukosekana kwa usimamizi mazuri wa kiongozi huyo
kumesababisha barabara nyingi za mkoa huo kuwa chini ya kiwango na
nyingine kuharibika muda mfupi baada tu ya kutengenezwa.
“Ameshindwa
kusimamia lakini anakuwa mtu wa kwanza kudai fedha za kuwalipa
wakandarasi ambao wamejenga barabara chini ya viwango angepaswa
kusimamia atakapokwama au kumuona mkandarasi ameshindwa kufanya kazi
yake kwa viwango basi angenieleza ili tuone tunafanya utaratibu gani,” alisisitiza.
Makonda pia alisema ni jukumu la kila kiongozi kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kuwa msimamizi mkuu katika idara yake.
“Hatutomvumilia
kiongozi yeyote atakayekwenda kinyume na taratibu za kazi inavyomtaka
kama ameshindwa bora ahame mkoa kwa sababu hapa kwangu sitamvumilia,” alisema
No comments:
Post a Comment