Na Othman Khamis Ame, OMPR
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahakikishia
wananchi wote kwamba Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itabakia kuwa ya amani na utulivu ili kuwapa nafasi wananchi wake
waendelee na harakati zao za kimaisha kama kawaida.
Alisema
Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kamwe haitakubali
kuona amani iliyopo anatokea mtu au kikundi kinachojaribu kuichezea
amani hiyo na kuhatarisha maisha ya watu.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Makamishna na
watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) mara baada ya
kupokea nakala ya Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania kutoka
kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Staafu Mh. Daniel Lubuva.
Balozi
Seif alisema uchaguzi wa Zanzibar kwa sasa umeshakamilika kwa mujibu
wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 sura ya Tisa kifungu cha 118
iliyoipa mamlaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuendesha uchaguzi bila ya
kuchukuwa amri au maelekezo kutoka kwa mtu ye yote.
Alisema
kazi iliyopo mbele kwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla ni kufanya
kazi kwa juhudi na maarifa huku wakijianda kwa uchaguzi mwengine
ifikapo mwaka 2020.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi na Watendaji wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Tanzania { NEC } kwa kazi kubwa na nzito ya kusimamia
uchaguzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na
Madiwani na kumalizika zoezi kwa salama na amani.
Mapema
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Msaafu Mh. Daniel
Lubuva alisema pamoja na jukumu la Tume hiyo kuendelea kusambaza
Taarifa za Tume hiyo ya mwaka 2015 kwa Viongozi Wakuu lakini watendaji
wake bado wana kazi ya kujiandaa na uchaguzi mwengine ujao wa Mwaka
2020.
Jaji
Mstaafu Lubuva alisema sheria ya Kura ya Maoni nambari 11 ya Mwaka 2013
itaangaliwa upya kwa pamoja kati ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Tanzania { NEC} na ile ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } ili
kuona mapungufu yanayohitaji kufanyiwa marekebisho.
Alisema
Kura ya Maoni itapigwa kama Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
ilivyofafanua baada ya pande hizo mbili kupitia mapungufu hayo na
baadaye kupendekeza mswaada wa marekebisho yatakayopelekwa Bungeni kwa
hatua zaidi za kisheria.
Jaji
Lubuva alifahamisha kwamba Kauli ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ya kuendeleza Kura ya Maoni itaondoa
shaka kwa Watanzania waliokuwa wakifikiria kwamba zoezi hilo limefifia.
Mwenyekiti
huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania ameelezea faraja yake
kutokana na uhusiano wa karibu wa kikazi uliopo kwa muda mrefu kati ya
Tume anayoiongoza na ile Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC),
No comments:
Post a Comment