Wakati
Bunge likiwa limepitisha sheria ya uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi
nchini, Jukwaa la Haki Jinai ambalo linajumuisha Taasisi za umma na
serikali limekutana kujipanga namna zitakavyoweza kufanya kazi kwa
ufanisi kwenye Mahakama hiyo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison
Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma,
mara baada ya kufungua kikao hicho cha kazi cha siku mbili cha jukwaa
hilo.
Dk.
Mwakyembe alisema jukwaa hilo limehudhuriwa na viongozi wote wa Taasisi
ambazo zipo kwenye mfumo wa haki jinai ikiwemo Jeshi la Polisi, Usalama
wa Taifa, Mahakama, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(Takukuru).
Alisema
kikao hicho kinafanyika kipindi muafaka kwa sababu jana Bunge
lilipitisha muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali ambao unatoa
mwanya wa kuanzisha mahakama ya mafisadi na makosa ya rushwa.
Alibainisha
vyombo hivyo vinaangalia jinsi gani kimoja kimoja kwa ushirikiano
vitakavyoweza kufanikisha uanzishaji wa Mahakama hiyo.
Kikao
hicho kilihudhuriwa na idara ya polisi ambayo inatakiwa ipeleleze
haraka, Takukuru ifanye uchunguzi kwa haraka, Timu ya DPP na waendesha
mashtaka wake wote ifanye kazi kwa ufanisi sana kesi zisikae, Mahakama
nayo kama kuna vitu vinakwamisha vitatuliwe.
Alisema
chombo hicho kinatafakari namna vyombo hivyo vitakavyoshirikiana ili
mahakama hiyo iweze kufanya kazi kwa ufanisi kama Rais alivyoahidi.
Hata hivyo alisema pamoja na hilo wanajadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usimamiaji wa haki jinai nchini.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,Buswalo Mganga alisema
changamoto zinazoikabili haki jinai nchini ni uhalifu ambao unafanywa na
watanzania wenyewe na miongoni mwao wengine wanatoka nje na
washirikiana na watanzania na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment