Wakazi wa Jiji la Mwanza Wapongeza Uamuzi wa Rais Magufuli Kutumia Hela za Sherehe za Muungano Kupanua Barabara Ya Airport - LEKULE

Breaking

7 Apr 2016

Wakazi wa Jiji la Mwanza Wapongeza Uamuzi wa Rais Magufuli Kutumia Hela za Sherehe za Muungano Kupanua Barabara Ya Airport


Wakazi  wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wamempongeza Rais John Magufuli kwa hatua aliyochukua ya kuahirisha maadhimisho ya siku ya Muungano na kuokoa zaidi ya Sh bilioni mbili na kuagiza fedha hizo zitumike kufanya upanuzi wa Barabara ya Ghana kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Pamoja na pongezi hizo, wamemuomba Rais Magufuli baada ya barabara hiyo kukamilika kufanyiwa upanuzi, ipewe jina la “Barabara ya Muungano” kama njia ya kuienzi kauli yake hiyo aliyoitoa kwa wakazi wa jiji hilo.

Rais Magufuli akiwa Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko, juzi alitangaza kuahirisha maadhimisho ya siku ya Muungano mwaka huu na kuagiza fedha ambazo zingetumika kwa vinywaji, halaiki, gwaride na vyakula ambazo ni zaidi ya Sh bilioni mbili, zitumike kufanya upanuzi wa Barabara ya Ghana – Airport.


Kadhalika alielekeza siku hiyo iwe siku ya mapumziko ya kawaida kwa Watanzania kuiadhimisha wakiwa katika shughuli zao binafsi.

No comments: