Wabunge
wa bunge la Arika Mashariki, (EALA), kutokaTanzania, wameendelea na
ziara yao ya kutembelea vyombovya habari hapa nchini, ikiwa ni mkakati
wa Jumuiya hiyo, kushirikisha vyombo vya habari ili
kuwafahamishawananchi wa nchi hizo manufaa ya jumuiya hiyo kwao.
LeoAprili 13, 2016, wabunge hao wakiongiozwa na Mwenyekiti wao Mh.
Makongoro Nyerere, wametembelea kampuni ya The Guardian, wachapishaji wa
magazeti ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha, na kupata fursa ya
kuelezwa shughuli zifanywazo na waandishi wa habarikwenye kampuni hiyo
ambapo walitembelea kitengo cha habari mtandao, (E-NEWS), kitengo cha
usanifu gazeti na kumalizia kwa mkutano wa kubadilishana mawazobaina ya
wabunge hao na uongozi wa chumba cha habari cha The Guardian. Pichani,
msanifu wa gazeti la The Guardian, Ben Mgana (aliyekaa), akiwaonyesha
jinsi gazeti hilo linavyoandaliwa kabla ya kuchapishwa. Wakwanza kushoto
ni Mhari Mtendaji wa gazeti hilo, Wallace Maugo, Mkuu wa chumba cha
Habari cha The Guardian, Jesse Kwayu, (wapili kushoto) na wabunge wa
hilo wakiongozwa na wmenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere (watatu kulia).NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MhaririMtendaji
wa The Guardian, Wallace Mauggo, (watatu kushoto) na Mhariri Mkuu wa
Chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu)
wakiwaonyesha wabunge hao baadhi ya magazeti yanayochapishwa na kampuni
hiyo
Mwenyekiti
wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, 9wapili kulia),
akisalimianana Mkuu wa kitengo cha habari mtandao (E-NEWS), cha The
Guardian Limited, Mashaka Mgeta, wakati wabunge hao walipotembelea
chumba cha Habari cha The Guardian Mikocheni jijini Dar es Salaam
Mashaka(kushoto) akisalimiana na Mbunge Mh. Nderakindo Kessy
Mauggo (kushoto), akitoa maelezo kwa wabunge hao
"Sisi
The Guardian, tukotayari kushirikiana na wabunge wa EALA, katika
kuujulisha umma kuhusu manufaa ya jumuiya na nitoe wito kwa mbunge mmoja
mmoja au kwa kupitia kundi lenu, mpatabo jambo muhimu mnalotaka jamii
ilifahamu msisite kutujulisha nasi tutashirikiana nanyi" Jesse Kwayu
(kushoto). Anayemsikiliza ni Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh.
Makongoro Nyerere.
"Tuko
tayari kuweka column maalum kwa ajili ya shughuli za Jumuiya ya Afrika
Mashariki, miongoni mwenu mnaweza kuchangia kwa kuandika" Wallace
Mauggo
"Lazima tukienzi Kiswahili ninampongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha njia" Mh. Nderaikindo Kessy
"Waambieni
Watanzania waondokane na uoga ni wakati muafaka sasa kwa wananchi wa
Jumiya ya Afrika Mashariki kushiriki katika fursa za kiuchumi katika
mfumo wa soko la pamoja, ili wmananchi wa Kigoma aweze kuvuka mpaka na
kuingia Bunjumbura kuuza mihogo yake" Mh. Makongoro Nyerere
"Tunaomba
ushirikiano zaidi wa vyombo vya habari katika kutangaza fursa za
kiuchumi zilizoko kwenye Jumuiya lakini pia ninaomba tuungane pamoja
katika kuhakikisha Kiswahili inakuwa lugha rasmi ndani ya bunge la
Afrika Mashariki." Shy-Rose Bhanji
Jesse akisikiliza kwa makini
Mh. Bernard Murunya (kulia), akimuonyesha kitu Mashaka Mgeta
Picha
ya pamoja, kutoka kushoto), Mh. Nderaikindo Kessy (Mb), Mh. Bernard
Murunya (Mb.), Bw. Wallace Mauggo (Mhariri Mtendaji The Guardian), Mh
Twaha Taslima (Mb), Bw. Jesse Kwayu, (Mkuu wa chumba cha Habari The
Guardian Ltd), Mh. Makongoro Nyerere (Mwenyekiti wa wabunge wa
EALA-Tanzania), Mh.Maryam Mohammed (Mb),Mh. Shy-Rose Bhanji (Mb) na
Bw.Asheri Michael
Jesse (kushoto), Mh. Makongoro Nyerere, na Bw. Wallace Mauggo
Mh. Nderaikindo Kessy
Mh. Bernard Murunya (kushoto) na Mh. Maryam Mohammed
Mh. Maryam Mohammed
Mh. Twaha Mussa Taslima, (kushoto) na Mh. Shy-Rose Bhanji
Wabunge
kutoka kulia, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Twaha Mussa Taslima, Mh.
Makongoro Nyerere, Mh. Maryam Mohammed, Bw.Asheri Michael wakimsikiliza
MhaririMkuu wa chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse
Kwayu
No comments:
Post a Comment