Yanga wameimaliza Mwadui FC wanaisubiri Mtibwa Sugar mchezo wa kiporo - LEKULE

Breaking

13 Apr 2016

Yanga wameimaliza Mwadui FC wanaisubiri Mtibwa Sugar mchezo wa kiporo


April 13 klabu ya Dar es Salaam Young Africans iliendelea na harakati zake za kumaliza viporo vya mechi za Ligi Kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ilikuwa na viporo vitatu ila April 13 2016 imemaliza mchezo wake wa pili wa kiporo dhidi ya klabu ya Mwadui FCya Shinyanga.
Yanga waliingia uwanjani wakiwa wanajua umuhimu wa mchezo dhidi ya Mwadui FC, kwani ilikuwa ni lazima wapate point tatu ili wajiweke katika nafasi nzuri, Yangawalifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika ya 4 na Haruna Niyonzima dakika ya 87, wakati Mwadui FC waliambulia goli la kufutia machozi kupitia kwa Kelvin Sabato dakika ya 14.
DSC_0079
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha jumla ya point 56 wakiwa nyuma ya watani zao wa jadi Simba walio nafasi ya kwanza wakiwa na point 57 lakini wameizidi Yanga mchezo mmoja pekee. Yanga watashuka tena dimbani April 16 2016 kucheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

No comments: