MABORESHO YA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA NDIO MKOMBOZI WA SIASA NCHINI- WAZIRI MHAGAMA. - LEKULE

Breaking

13 Apr 2016

MABORESHO YA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA NDIO MKOMBOZI WA SIASA NCHINI- WAZIRI MHAGAMA.

 Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji francis S. K Mutungi pamoja na Maaafisa Wandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa nje ya ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam Leo kabla ya kuanza kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
  Dkt. Abdallah Possi, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu) Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu akiteta jambo na Msajili wa vyama vya Siasa  Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi  kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
 Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,  Jaji Francis S.K Mutungi akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti yam waka 2016/2017 ya  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Manaibu waziri ,Mhe Antony P. Mavunde na Mhe. Dkt Abdallah Possi.
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kulia ni Mhe. Dkt Abdallah Possi, Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu .
 Angelina Sanga, Katibu kiongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria akiwapitisha wajumbe (hawapo pichani) kwenye vifungu vya bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe Richard Ndassa  akiwasilisha hoja kwenye  kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kulia ni wajumbe wa kamati.

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Sheria wamepewa rai ya kushikamana na Serikali katika kuhakikisha kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka1992 na Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 yanafanyika ili kuondoa utata na migongano ya utekelezaji wa masuala ya siasa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akijibu swali kutoka kwa wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam ambao walihoji uhalisia wa utekelezaji wa sheria zililizopo sasa.

Wajumbe hao walihoji utitiri wa vyama vingi nchini ambavyo miaka nenda rudi havina madiwani wala wabunge na vingine kutoshiriki katika chaguzi . Wajumbe pia walihoji gharama ndogo za usajili wa vyama vya siasa ukilinganisha na hali ya maisha iliyopo kwa sasa.
Jambo lingine ambalo wajumbe wamehoji ni nafasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika kushughulikia migogoro ya kisiasa ndani na nje ya Vyama vya Siasa na ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi ndani ya vyama vya siasa.

Akijibu hoja hizo Mhe Mhagama amesisitiza kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za uchaguzi ndio njia pekee itakayompa meno Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo.


 “Sheria tulizonayo ndio inatoa mwanya wa haya yote haya na ndio maana Serikali kwa sasa inaendelea na taratibu za kuboresha sheria hizi, tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ameshawasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Vyama vya Sasa na Sheria ya gharama za uchaguzi na sisi tumeridhia , tunasubiri tu bunge kujadili ili ziweze kutumika”alisisitiza mhe Mhagama.

No comments: