Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,
akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe, wakati
walipowasili kwenye viwanja vya Karimjee, kulikofanyika shughuli ya
kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai,
ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu
Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na
Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.Kushoto ni Mke wa Rais, Mama
Jannet Magufuli
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini
kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye
alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mkewe
Mama Jannet Magufuli, wakisalimiana na baadhi ya waheshimiwa wabunge
waliokuwepo kwenye shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa
Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum
kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es
salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpa
pole, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe, kufuatia msiba wa
Mbunge wa Chama chake, Marehemu Christina Lissu Mughwai.
Mwili
wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti
Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ukuwasili
kwenye ukumbi wa Karimjee leo, Jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpa, akimfariji Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, akimfariji Mh. Tundu Lissu, Mbunge
wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina
Lissu Mughwai.Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson,
akifuatiwa na Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina
Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa
shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar
es salaam.
Mtoto wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Veronica Mallya akitoa taarifa fupi juu ya Mama yake.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli,
akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa
ya Mama yake.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa
heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye
alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu
Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki
iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akiagana Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.
No comments:
Post a Comment