Michezo ya viporo ya Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea kupunguzwa kwa upande wa klabu ya Azam FC ya Mbande Chamazi, Azam FC leo April 6 2016 imecheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya klabu ya Ndanda FC wanakuchele kutokea Mtwara.
Kwa taarifa za awali huu ni mchezo ambao awali Azam FC
waliomba usogezwe mbele ili waendelee na michuano yao ya Kombe la
Shirikisho barani Afrika lakini hawakukubaliwa, hivyo wakaamua kuendelea
na mchezo huo, Azam FC ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani imeambulia sare ya goli 2-2, hii ni sare ya pili mfululizo kwa Azam FC baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na Toto African weekend iliyoisha.
Azam FC walianza kwa kupata goli la uognozi dakika ya 16 kupitia kwa Ramadhani Singano na Didier Kavumbagu dakika ya 42, ila mambo yalibadilika kuanzia dakika ya 52 baada ya Atupele Green kufunga goli la kwanza kwa Ndanda FC, kwani Ndanda walionekana kuishambulia sana Azam FC na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa kitu ambacho kilipelekea Aggrey Morris kujifunga goli dakika ya 88 na mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.
No comments:
Post a Comment