KAMATI ya
Bunge ya Kudumu Huduma za Maendeleo ya Jamii mapema leo Aprili 5.2016
imetembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road na kujionea uendeshaji
unaoendelea katika taasisi hiyo ikiwemo pia kuangalia jengo maalum
litakalowekwa mitambo ya mionzi ya taasisi hiyo.
Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba
(Mbunge) pamoja na wajumbe mbalimbali wa kamati huku wakibaini
changamoto ikiwemo ukosefu wa dawa zinazoikabili taasisi hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk.
Julius Mwaiselage katika taarifa yake kwa Kamati hiyo aliweza kubainisha
changamoto mbalimbali zinazoikabili Ocean Road ikiewemo suala hilo la
madawa na bajeti wanayoomba Serikali kwani uendeshaji ni mkubwa na
kiwango wanachokipata ni kiasi wastani katika maobo yao hayo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla aliweza kutoa maelezo ya Wizara
yake hiyo ya Afya namna walivyojipanga kusaidia taasisi hiyo huku
akiahidi kuyashughulikia matatizo yote kadri inavyowezekana.
Aidha, Wananchi wakiwemo ndugu wa wagonjwa wanaouza wagonjwa wao
waliweza kumvamia Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla kwa lengo la
kutaka kutatuliwa kero zao hasa suala la ukosefu wa dawa Hospitalini
hapo ambapo walimuomba atatue tatizo hilo haraka.
Wananchi hao licha ya kupongeza huduma zitolewazo Hospitalini hapo
na taasisi hiyo, tatizo lao kubwa ni ukosefu wa dawa kwani hali imekuwa
ni ngumu kwa muda mrefu kwa wao kutafuta dawa nje ya taasisi hiyo na
huko wanapozipata ni kwa bei kubwa.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage
(katikati) akiwa na wajumbe wa Bunge kamati ya Maendeleoya Jamii
walipotembelea jengo jipya la taasisi hiyo linalojengwa kwa ajili ya
kufunga mashine za mionzi.
Mbunge
Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEA, Mh. Joseph Mbilinyi 'Sugu (Kulia)
akiwa na wajumbe wengine wakitoka katika kuangalia jengo maalum
linalojengwa kwa ajili ya kufungwa mashine za mionzi za kupimia ugonnjwa
wa saratani.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiingia katika jengo la taasisi hiyo ya Ocean Road..
Wajumbe wa Kamati ya Bunge wakiendelea na kikao hicho
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius
Mwaiselage akisoma taarifa ya taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Maendeleo ya Jamii
Wajumbe wakiuliza maswali juu ya mwenendo wa taasisi hiyo
Kikao hicho kikiendelea..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu maswali hayo yaliyoulizwa Wizara yake
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo ya kina juu ya maswali
yaliyoulizwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii..
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage (wa
pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na watendaji wa kuu wa taasisi hiyo
muda mfupi baada ya kuagana na Naibu Waziri Dk. Kigwangalla (hayupo
pichani).
Wananchi wakimsimamisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla kijibu kero mbalimbali
katika taasisi hiyo ya Ocean Road
Wananchi wakimuuliza mawali Naibu Waziri juu ya kero wanazokabiliana nazo katika taasisi hiyo wanapofika kupatiwa matibabu
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu akitoa majibu kwa wananchi hao ambao
wanapatiwa matibabu na wengine walifika kuangalia ndugu zao wanaopatiwa
matibabu katika taasisi hiyo ya Ocean Road.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (katikati mwenye suti) akikatiza mitaa
ya Ocean Road kurejea Ofisini kwake Wizara ya Afya baada ya kumaliza
majukumu yake ya kikazi ikiwemo kuambatana na Kamati ya Bunge Huduma za
Maendeleo ya Jamii iliyotembelea katika taasisi hiyo ya Ocean Road.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti) akirejea kwa miguu
kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuelekea Wizarani kwake kwa
miguu... (Picha zote na Andrew Chale).
No comments:
Post a Comment