Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii yatembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya TBC-Kisarawe. - LEKULE

Breaking

1 Apr 2016

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii yatembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya TBC-Kisarawe.

 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii wakipitia taarifa ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe pwani na maendeleo yake.
Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha  taarifa ya shirika hilo  kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba.Picha na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
   Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Bw.Peter Serukamba katika viwanja vya urushaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Kisarawe

No comments: